Askari wamemtia mbaroni mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 30. Mwanamke huyu anadaiwa kumuua mwanawe wa miaka mitatu kwa kumpa sumu katika kaunti ya Migori.
Akizungumza, kamanda wa polisi katika kaunti hiyo,Joseph Nthenge amesema kuwa mshukiwa huyo anayefahamika kama Faith Akinyi alijaribu kunywa sumu hiyo lakini alinusurika kifo alipofikishwa hospitalini.
READ ALSO: Waziri wa fedha matatani
Katika barua iliyopatikana katika nyumba ya mshukiwa huyo,Faith amedai kuwa chanzo cha yeye kutaka kuyachukua maisha yake ni kuwa mumewe ameitelekeza familia yake.
Mwanamke huyo anadaiwa kuwa alimpa sumu mwanawe kisha akanywa sumu hiyo mwenyewe kabla ya wawili hao kupelekwa katika hospitali ya Akidiva ambapo mwanawe alifariki.
Kulingana na familia ya mwanamke huyu, sio mara ya kwanza kwa mwanamke huyo kujaribu kuyachukua maisha yake.