Mnamo Agosti tarehe 11, Martin Shikuku Alukoye, alizikwa akiwa na sare zake za huduma ya vijana wa kaunti ya Kakamega baada ya kufa maji.
Siku moja baadaye, maafisa wa eneo hilo la Kakamega waliiandama familia yake wakitaka sare za huduma ya vijana alizozikwa nazo.
Baada ya na familia hiyo kupinga ombi hilo, maafisa hao waliufukua mwili wake na kuchukua sare hizo.
Akizungumza, mjomba wa mwendazake amesema kuwa maafisa hao wamekiuka tamaduni zao na sheria za nchi kwa kuufukua mwili wake bila amri ya korti.
TAZAMA PIA: Mwanamke amuua mwanawe http://www.kdrtv.co.ke/swahili/mwanamke-amuua-mwanawe/
Naibu wa chifu katika eneo la Ituti ameahidi kuchukua hatua kali dhidi ya maafisa hao kwani lazima mtu awe na amri ya korti ili aweze kuufukua mwili wa mtu yeyote.
Mwili huo ulivishwa nguo na kuzikwa tena baada ya familia ya mwendazake kufanyiwa tambiko za utakaso.