SEHEMU ya wabunge kutoka eneo la Mlima Kenya wamepinga madai kwamba mawaziri kutoka eneo hilo wamekuwa na njama ya kumwangamiza Naibu rais, William Ruto.
Kwa mujibu wa wabunge hao watetezi, wanaoibua madai hayo wana malengo ya kuchochea jamii nyingine nchini Kenya kutenga Mlima Kenya, huku wakisisitiza kwamba mawaziri hao hawajafanya mpango wowote wa mauaji.
Wabunge hayo waliongozwa na mbunge wa Neyri mjini Ngunjiri Wambungu wengine wakiwemo Ruth Mwaniki (Kimumo), Joseph Nduati (Gatanga), Maoka Maore (Igembe),Gathoni Wamuchonba (Kiambu) na mbunge wa Kiambaa Paul Koinange.
Aidha, madai hayo ya mauji yameibua hisia mbali mbali miongoni mwa wakenya, huku wengine wakishikilia kwamba barua iliyoenezwa mitandaoni yana ukweli fulani. Kwa upande mwingine, kunao wakenya ambao wanasema kwamba madai hayo ni ya kuyumbisha uongozi wa Rais Uhuru Kenyatta.