Waziri wa fedha Hery Rotich na katibu wake Kamau Thugge wamejisalimisha kwa makachero wa DCI Nairobi.
Bwana Henry Rotich yuko kati ya maafisa wengine 26 ambao imeamrishwa na mkurugenzi wa mashtaka ya umma, Noordin Haji, wakamatwe.
Watu hao wamekamatwa kufuatia tuhuma ya kuwa wamehusishwa katika sakata ya mabwawa ya Kimwarer na Arror.
Kati ya wengine ambao wamekamatwa ni kaimu afisa mkuu wa shirika la KVDA Francis Kipkech na David Onyango.
Washukiwa wengine katika sakata hiyo ni katibu katika wizara ya Afrika Mashariki Susan Kipkoech, mkurugenzi wa Nema Geoffrey Wakhungu, Kennedy Nyachiro na Jackson Kinyanjui wote kutoka wizara ya fedha, Moses Kipchumba, Nelson Korir, Isaac Kiiru, Patrick Kipsang, Frederick Towett, Jotham Ruto, Charity Muui, na David Ongare walioketi kwenye kamati ilioidhinisha kandarasi ya ujenzi wa mabwawa hayo ya Arror na Kimwarer.
Kulingana na Bwana Noordin, upo ushahidi wa kutosha unaoonyesha kuwa watu hawa walihusika katika kupora fedha hizo.
Wakifikishwa mahakamani watajibu mashtaka ya kutumia ofisi za umma vibaya na kujihusisha katika njama ya kutapeli pamoja na mashtaka mengine.
k